Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 04Article 540958

Habari za michezo ya

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kahata, Chikwende ‘bye bye’ Simba!

Kahata, Chikwende ‘bye bye’ Simba! Kahata, Chikwende ‘bye bye’ Simba!

SIMBA imeshampa taarifa ya kuachwa winga Mkenya, Francis Kahata huku ikiwa kwenye mchakato wa kufanya hivyo pia kwa Mzimbabwe, Perfect Chikwende.

Awali, uongozi wa Simba uliondoa jina la Kahata katika mashindano ya ndani na kumtumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo wameishia katika hatua ya robo fainali baada ya kuondolewa na Kaizer Chiefs.

Kutokana na Simba kumuondoa Kahata katika mashindano ya ndani na kutolewa katika Ligi ya Mabingwa maana yake mchezaji huyo yupo ndani ya timu bila ya matumizi yoyote.

Mtoa taarifa huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa tayari ndani ya wiki hii alikutana na viongozi na wakakubaliana Kahata kulipwa kila ambacho anastahili kutokana na mkataba wake ulivyo na baada ya hapo kumpa tiketi ya kurudi kwao Kenya Jumapili hii.

Awali kocha wa Simba, Didier Gomes aliwahi kuliambia Mwanaspoti moja ya mchezaji ambaye anavutiwa naye kutokana na utendaji wake wa kazi uwanjani ni Kahata.

Kuhusu Chikwende ambaye wamemsajili dirisha dogo akitokea FC Platinum ya Zimbabwe naye safari imeiva. Simba walimsajili Chikwende baada ya kuwafunga bao moja katika mechi ya mzunguko wa kwanza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na kiwango bora alichoonyesha katika michezo yote miwili.

Related Ajibu apewa masharti manneChikwende baada ya kusajiliwa na Simba alichukua nafasi ya Kahata kucheza mashindano ya ndani lakini hakutumika mara kwa mara.

“Kuna uwezekano Chikwende akatolewa kwa mkopo katika moja ya timu ya nje ya Tanzania,” kilisema chanzo.

Join our Newsletter