Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 14Article 542533

Habari za michezo of Monday, 14 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kaizer Chiefs Wafunguka Dili la Kambole Yanga

Kambole Kambole

WAKATI Yanga ikiwa kwenye harakati za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji matata wa Kaizer Chiefs, Mzambia, Lazarous Kambole, uongozi wa Kaizer Chiefs umetoa neno juu ya dili hilo.

Ipo hivi; Inafahamika kuwa, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said yupo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanikisha dili hilo, baada kumalizana na beki wa AS Vita, Djuma Shabani kwa mkataba wa miaka miwili.

Spoti Xtra linafahamu kila kitu juu ya dili la mshambuliaji huyo ambapo Kaizer wapo tayari kumuachia kutokana na kushindwa kuonesha ubora wake tangu alivyojiunga na timu hiyo mwaka 2019 akitokea Zesco United ya Zambia.

Kambole ameliambiaSpoti Xtra kuwa: “Sina sababu ya kudanganya juu ya hilo, lakini ukweli sijui kitu chochote kinachoendelea.

”Alipotafutwa meneja wa mawasiliano wa timu hiyo, Alpheus Maphosa ‘Vina’ juu ya kuzungumzia hilo, kwanza alionesha ukali akisema: “Siwezi kukubali kuongea na mwandishi iwe kwenye ukweli au uongo, naomba unithibitishie hizo taarifa za tetesi umezitolewa wapi.”

Baada ya kuthibitishiwa taarifa hizo juu ya Yanga kumtaka Kambole, akaibuka na kusema: “Unajua viongozi wa Kaizer wapo bize na mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sasa kama dili la mchezaji likiwa limekamilika nitakueleza mapema.”

IBRAHIM MUSSA NA MUSA MATEJA, DAR