Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 23Article 553249

Soccer News of Monday, 23 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Kama yanayosemwa yangekua ya kweli, Yanga ilipaswa kupongezwa" - Bumbuli

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli

Klabu ya Yanga imeamua kuvunja kambi yake iliyokuwa imeweka nchini Morocco na itarejea nchini kuanzia kesho mchana majira ya saa saba kwa saa za Afrika Mashariki.

Sababu ya kufanya hivyo zimewekwa wazi na Mtu wa ndani kabisa kutoka klabu ya Yanga, Injinia Hersi na baadae Klabu ya Yanga imetoa taarifa rasmi juu ya suala hilo.

Lakini kuna taarifa zimekua zikisambaa kwa kasi na hasa katika mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya Wachezaji wamekutwa na Maambukizi ya Virusi vya Corona, na ndio sababu ya Kambi hiyo kusitishwa.

Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli ametoa taarifa juu ya suala hilo;

"Nadhani taarifa rasmi imejieleza ila kama ni kweli ingekua hivyo inavyosemwa nadhani Klabu ya Yanga ilipaswa kupongezwa"

"Maana ingekua imechukua hatua madhubuti kulinda wengine, watu wanataka kufanya kama Corona ni ugonjwa wa aibu au fedheha hivi, cha msingi niwaombe wanayanga wajihadhari Corona ipo na Siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi waje wamevaa barakoa" amesisitiza Bumbuli

Yanga inajiandaa kwa Tamasha kubwa la wiki ya Mwananchi ambalo litafanyika katika Uwanja wa Kumbu kumbu ya Benjamin Mkapa Agosti 29.