Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 12Article 542404

Habari za michezo of Saturday, 12 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kamati TFF: Tunafuata kanuni

Kamati TFF: Tunafuata kanuni Kamati TFF: Tunafuata kanuni

KAMATI ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema katiba na kanuni za uchaguzi haziwezi kufanyiwa marekebisho wakati mchakato unaendelea.

Akizungumza na gazeti hili jana mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Wakili Kiomoni Kibamba alisema yapo maoni mengi kutoka kwa watanzania kuhusu mchakato wa uchaguzi ushauri wao ni kuendelea kufuatilia kwa vile mchakato unaendeshwa kwa kufuata miongozo iliyopo ambapo ni katiba ya TFF pamoja na kanuni za uchaguzi za Shirikisho hilo.

“Mwitikio wa wagombea hasa nafasi ya urais ni mzuri hivyo tunatoa wito kwa wanafamilia wenye nia ya kugombea kutumia siku iliyobaki kuchukua na kurejesha fomu,” alisema Wakili Kibamba.

Leo ndio mwisho wa kuchukua fomu kwa wanaowania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Tanga Agosti saba mwaka huu.

“Wagombea waliotuandikia kuomba mwongozo au kutupa maelekezo yao kuhusu uchaguzi huu tumewapa majibu kwa maandishi na kama zilivyo katiba au kanuni za uchaguzi haziwezi kufanyiwa marekebisho wakati mchakato unaendelea,” alisema Wakili Kibamba.

Wakati huo huo Hawa Mniga, Ally Saleh na Rahim Zamunda wamechukua fomu ya kugombea urais.

Mniga, Saleh na Zamunda wanaungana na Wallace Karia, Evans Mgeusa, Zahor

Haji, Oscar Oscar, Deogratius Mutungi, Abbas Tarimba na Ally Mayay kuwania nafasi hiyo.

Katika nafasi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochukua fomu ni Ellyson Mweladzi na Jimmy Shomari kupitia

Kanda namba moja ya mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Morogoro na Pwani akiungana na Lameck Nyambaya, Liston Katabazi na Michael Petro, Saady Khimji na Athuman Kambi.

Wengine ni Zakayo Mjema kupitia Kanda namba mbili ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga akiungana na Khalid Abdallah.

Kanda namba tatu ya mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma na Songwe wamechukua Abousufian Sillia, James Mhagama na Joseph Nganungwa.

Kanda namba nne ya mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Dodoma na Singida waliochukua ni Mohamed Aden, Osuri Kosuri na Hamisi Juma.

Vedastus Lufano na Salum Chama wamechukua kupitia kanda ya tano ya mikoa ya Geita, Kagera, Mara na Mwanza.

Kanda namba sita ya mikoa ya Katavi, Kigoma, Rukwa na Tabora waliochukua ni Blassy Kiondo na Issa Bukuku.