Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 24Article 553477

Soccer News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kambi ya Simba kuna jambo

wachezaji wa Simba SC wakiwa gym wachezaji wa Simba SC wakiwa gym

Huku kambi ya Simba huko Rabat, Morocco ikizidi kunoga kwa mastaa kuendelea kufanya mazoezi mara mbili kwa siku, imeelezwa kwamba kambi hiyo inaweza kuvunjwa muda wowote.

Simba wanafanya mazoezi hayo magumu asubuhi gym na jioni mazoezi ya uwanjani ambayo ni ya ufundi zaidi.

Kocha wa timu hiyo, Didier Gomes alisema amefurahishwa na kambi hiyo kwani kila mchezaji ameonyesha ari na morali ya kujituma kwa kiasi kikubwa.

Katika hatua nyingine inaelezwa kambi ya Simba inaweza kuvunjwa huko Morocco kutokana na wachezaji wengi kuitwa kwenye timu zao za taifa na kuna makundi mawili tayari yametangulia kuondoka.

Kundi la kwanza ambalo limetangulia lipo na wachezaji wanane ambao wanacheza timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na tayari wamewasili nchini kwa ajili ya kambi hiyo inayoanza leo Jumanne.

Wachezaji hao ni John Bocco na Aishi Manula na kuifanya Simba ibaki na kipa mmoja tu Ally Salim ambaye ndio alicheza mechi ya kirafiki na AS Rabat iliyo chini ya kocha, Sven Vandenbroeck huku Beno Kakolanya akirudi nchini baada ya kufiwa na mama yake mzazi.

Kutokana na uchache huo wa wachezaji waliobaki kambini huenda kambi hiyo ikaahirishwa na wachezaji waliobaki watarudi nchini kwa ajili ya muendelezo wa sehemu ya maandalizi.

Inaelezwa wachezaji hao wa Simba, watarudi kwa makundi tofauti kama ambavyo waliondoka na kambi inaweza kuwekwa hapa Dar es Salaam au nje ya mkoa ili kuendelea na maandalizi yao ambayo Septemba 25, ambapo watacheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema wanaendelea vizuri na kambi lakini changamoto kubwa ambayo kwa sasa wanakutana nayo kikosi kupungua kwani timu yao ina wachezaji wengi wanaocheza timu za taifa ukiachilia mbali Taifa Stars, Kenya, Uganda na Zambia.

“Kiukweli kiufundi ni changamoto ila tutaangalia namna gani tunaendelea kuwa nao wachezaji waliobaki.”