Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 23Article 553234

Habari za michezo of Monday, 23 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kamwaga: Muda wangu Simba ukiisha naondoka

Kamwaga: Muda wangu Simba ukiisha naondoka Kamwaga: Muda wangu Simba ukiisha naondoka

KAIMU Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ezekiel Kamwaga ameweka wazi kuwa ataondoka katika nafasi hiyo mara tu baada ya muda aliopewa wa miezi miwili kukaimu kukamilika.

Julai 28, mwaka huu Bodi ya Wakurugenzi ya Simba ilimtangaza rasmi Kamwaga kushika nyadhifa ya Kaimu wa Idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo, kuifuatia kuondoka kwa aliyekuwa Msemaji wa Simba Haji Manara.

Akizungumzia na Mwanaspoti amesema majukumu yake ndani ya Simba Kamwaga alisema Watu wengi wamekuwa wakiuliza kwanini ana kaimu nafasi hiyo kwa miezi miwili pekee licha ya kwamba ana uzoefu wa kutosha wa kusalia kwa muda mrefu zaidi.

“Ningependa kuweka wazi makubaliano yangu na Uongozi wa juu wa Simba ni kushikilia nafasi hii kwa miezi miwili na baada ya hapo siwezi kuongeza hata siku moja mara baada ya muda huo kukamilika.

Kamwaga alisema kuwa sababu ya kutoongeza muda mwingine ni kutokana na majukumu yake binafsi ambayo anatakiwa kuyafanya nje ya Tanzania, hivyo kabla ya kuondoka lazima ahakikishe amekamilisha kazi ya kufanikisha mchakato wa kumtafuta msemaji mwingine mpya.