Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 10Article 584755

Habari za michezo of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kapombe: Tunaitaka Fainali Mapinduzi

Kapombe Kapombe

BEKI wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe, amefunguka kuwa wanataka kushinda mchezo wao wa nusu fainali wa Kombe la Mapinduzi kwa kuwa wanataka kuibuka mabingwa wa kombe hilo.

Timu hizo mbili zinakutana leo Jumatatu katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi hatua ya nusu fainali utakaopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kapombe amesema kuwa; “Tunauchukulia huu mchezo kwa umuhimu sana maana tukikosea tutatoka. Namungo tunawajua maana tumetoka kucheza nao kwenye lligi muda sio mrefu.

“Kama wachezaji wa Simba tumejipanga kuweza kupambana kwa hali ya juu ili kuweza kuingia fainali na kuweza kuchukua kombe.”