Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573235

Habari za michezo of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kassim Dewji amrithi Hans Poppe Simba

Kassim Dewji amrithi Hans Poppe Simba Kassim Dewji amrithi Hans Poppe Simba

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again amemtangaza Kassim Dewji kuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo.

Dewji anachukua nafasi ya Zacharia Hans Poppe aliyefariki miezi kadhaa iliyopita na kuzikwa mkoani Iringa.

Katika mkutano mkuu wa klabu hiyo leo Jumapili, Try Again amesema bodi imempendekeza Dewji kuchukua nafasi ya Poppe.

"Tunafahamu uwezo Dewji, hivyo bodi imemkabidhi jukumu la kuongoza kamati ya usajili ambayo ilikuwa ikiongozwa na Poppe enzi za uhai wake," amesema Try Again.