Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 09Article 584467

Soccer News of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kaze akusanya jeshi lake kuwakabidhi Azam, yupo mayele, Bangala na Saido

Yanga watakutana na Azam mchezo wa nusu Fainali Mapinduzi Cup Yanga watakutana na Azam mchezo wa nusu Fainali Mapinduzi Cup

Yanga imepania kutetea ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi baada ya kocha msaidizi wa timu Cedric Kaze kuita nyota wake kwa ajili ya mechi ya nusu fainali dhidi ya Azam.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho Jumatatu Uwanja wa Amaan uliopo kisiwa cha Unguja huku nyota Fiston Mayele, Yanick Bangala na Said Ntibayonkiza 'Saido' wakiongeza nguvu kikosini.

Hata hivyo Yanga kesho watawakosa nyota watatu Salum Abubakar 'Sure Boy' ambaye ana malaria, Denis Nkane na Yasin Mustafa wao waliumia mechi iliyopita.