Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 23Article 559189

Soccer News of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kaze atua Dar usiku wa manane

Cedrick Kaze (kulia) akiwa na Injinia Hersi Cedrick Kaze (kulia) akiwa na Injinia Hersi

Kocha Cedric Kaze tayari yupo nchini, ametua usiku wa kuamkia leo na huenda wakati wowote akatambulishwa kama Kocha Msaidizi.

Kaze ambae anahusishwa kujiunga na Kikosi cha Dar Young African kama kocha msaidizi.

Inaelezwa Kaze ataanza majukumu yake mara moja na atakuwa sehemu ya benchi la ufundi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii Jumamosi Septemba 25.

Kaze ameshawahi kuwa kocha Mkuu wa Yanga, kabla ya kuvunjiwa mkataba na kuachana nao mapema mwaka 2020.