Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 18Article 558145

Soccer News of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Kazi ni Moja tu Nigeria " - Yanga

Kikosi cha Yanga kimewasili salama nchini Nigeria, Tayari kuwavaa Rivers United Kikosi cha Yanga kimewasili salama nchini Nigeria, Tayari kuwavaa Rivers United

Timu ya Wananchi na mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu Tanzania Bara. klabu ya Yanga, imeondoka nchini jioni ya Septemba 17 kwa ndege ya Shirika la ATCL kuelekea nchini Nigeria.

Sasa tayari Klabu ya Yanga imeshatua Port Harcourt, Nigeria. Wasafiri wote wapo salama salmini na Uongozi wa klabu hiyo umedai kazi iliyobaki ni moja tu.Ushindi.

Yanga wana mchezo wa mkondo wa pili wa hatua za awali dhidi ya Timu ya Rivers United ya nchini Nigeria na tayari walishapoteza kwa goli 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza Jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Rivers United dhidi ya Yanga utapigwa siku ya Jumapili Septemba 19, ambapo wawakilishi hao wa Tanzania wamewaomba watanzania kuwaombea kwa kuwa ushindi utakapopatikana ni wa Taifa si Yanga pekee.