Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 26Article 544303

Habari za michezo of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kelvin John atua Genk

Kelvin John atua Genk Kelvin John atua Genk

MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania, Kelvin John ‘Mbappe’, amejiunga rasmi na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji ambayo nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, alikuwa akiichezea kabla ya kujiunga na Aston Villa ya nchini Uingereza.

Kelvin ambaye pia anaichezea timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Ngorongoro Heroes ya Tanzania, ni miongoni mwa vijana mwenye kipaji kikubwa kwani Mwaka jana aliorodheshwa na jarida la The The Guardian la nchini Uingereza kuwa miongoni mwa wachezaji wa kizazi kijacho.

Genk imethibitisha kumsajili mchezaji huyo kwa ushauri wa Samatta ambaye amekuwa rafiki yake wa karibu.