Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 27Article 554029

Habari za michezo of Friday, 27 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kesi ya Morrison yasogezwa mbele

Kesi ya Morrison yasogezwa mbele Kesi ya Morrison yasogezwa mbele

MAHAKAMA ya usuluhisho masuala ya mpira kimataifa ‘CAS’ imesogeza mbele hukumu ya kesi kati ya klabu ya Yanga dhidi ya mchezaji Benard Morrison iliyokuwa isikilizwe Agosti 26,2021.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na CAS  ikisainiwa na mshauri wao, Caroline Fischer imeomba radhi kwa pande zote mbili n kusogeza kesi hiyo mpaka Septemba 21,2021.

“Kwa niaba ya Rais wa mahakama ya usuluhisho (CAS) tunaomba pande zote mbili zipokee samhani ya kuchelewa kwa kutolewa rasmi maamuzi ya kesi, bado inafanyiwa kazi kwa kutoangalia upande wowote,”imesomeka taarifa hiyo iliyoandikwa na  Fischer.

Ikumbukwe Yanga walimfungulia kesi Morrison katika kamati ya Hadhi, Sheria za wachezaji kwenye Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) na kushindwa kesi hiyo ndipo wakafungua kesi nyingine CAS ambayo sasa hukumu yake itakuwa Septemba 21.