Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 21Article 543589

Habari za michezo of Monday, 21 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kibwana: Nitapigania namba na yeyote

Kibwana: Nitapigania namba na yeyote Kibwana: Nitapigania namba na yeyote

BEKI wa kulia wa Yanga, Kibwana Shomari amesema yupo tayari kupigania namba na mchezaji yeyote atakaye sajiliwa na timu hiyo.

Yanga inatajwa kumalizana na beki wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Djuma Shabani kutoka timu ya AS Vita na atajiunga na timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili jan, Kibwana alisema anafurahia usajili huo kwa kuwa utampa changamoto ya kupambana ili kupata nafasi ya kucheza na kupandisha kiwango chake.

“Nasikia Djuma Shabani amesaini Yanga na tutakuwa naye msimu ujao, ni jambo zuri kwa sababu anakuja kuboresha timu yetu na mimi nafurahi sababu nitajifunza vitu vingi kutoka kwake kutokana na uzoefu alionao, lakini sihofii kukosa nafasi ya kucheza sababu mwenye jukumu la kupanga timu ni kocha,” alisema Kibwana.

Mlinzi huyo ambaye alijiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar, alisema kucheza nafasi moja na wachezaji wakubwa kama huyo ni faida kwake hasa ikitokea ana mweka benchi hawezi kuchukia wala kufikiria kuondoka.

Alisema changamoto kama hizo ni za kawaida kwenye soka hata akiondoka Yanga atakapokwenda jambo kama hilo linaweza kumtokea hivyo ni bora akabaki na kupambania nafasi yake.