Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 10 06Article 561751

Soccer News of Wednesday, 6 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kibwana ilikua ni suala la muda tu Stars

Kibwana Shomari Kibwana Shomari

Wiki moja iliyopita Kocha Mkuu wa Kikosi cha Taifa Stars Kim Poulsen, aliita kikosi cha wachezaji 25, watakaoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kule Qatar 2022.

Jina la Kibwana Shomari halikuwepo, Kibwana ni beki wa pembeni wa Yanga, anacheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.

Mashabiki wengi walilalamika kuachwa kwa bwana mdogo huyo, lakini siku kadhaa mbele ameitwa, yeye pamoja na Kibu Denis.

Wadau wa masuala ya soka wamefunguka kuwa hata wao walishangaa kuachwa kwa beki huyo lakini walijua ni kwa muda tu na wakati mwingine atajumuishwa katika timu ya Taifa.

Wakimzungumzia beki huyo wamesema Kibwana kiumri bado ni mdogo sana hivyo bado ana muda wa kujifunza na kuimarika kila leo, anakubali kupambana, anakubali changamoto na mtu wa namna hiyo ni rahisi kuimarika, hivyo tulijua tu ataitwa wakati ukifika na hatimae ameitwa.

Stars itajitupa dimbani Oktoba 7, kupambana na Benin katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.