Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 25Article 553549

Habari za michezo of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kihamia Ajiuzulu Yanga

Kihamia Ajiuzulu Yanga Kihamia Ajiuzulu Yanga

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga, Dkt. Athuman Kihamia amejiuzulu nafasi hiyo jana Jumanne, Agosti 24, 2021.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kihamia amesema amechukua Uamuzi wa kujiuzulu ili kupumzika na kupisha wengine kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Hili limetokea mda mfupi tu mara baada ya Utambulisho wa Haji Manara.

“Wajumbe wenzangu habarini za jioni,nichukue nafasi hii kuwajulisha kuwa nimejiuzulu nafasi yangu.” amesema Dkt. Kihamia.