Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 22Article 547846

Habari za michezo of Thursday, 22 July 2021

Chanzo: millardayo.com

Kijana Gift alieuwawa kwa kupigwa Risasi DAR amezikwa leo (Picha 13+)

Kijana Gift alieuwawa kwa kupigwa Risasi DAR amezikwa leo (Picha 13+) Kijana Gift alieuwawa kwa kupigwa Risasi DAR amezikwa leo (Picha 13+)

Kijana Gift Mushi ambaye aliuwawa kwa kupigwa risasi akiwa Bar Sinza kwa Remy Dar es salaam weekend iliyopita, amezikwa leo kwenye makaburi ya Vikunai Mtoni Kijichi Dar es salaam.

Meneja wa Bar hiyo alisema Gift alipigwa risasi na Kijana mwenzake Alex Korosso baada ya kuinuka kutoka kwenye meza yake kwenda kumuomba Alex aache kutisha Watu kwa bastola aliyokua nayo ndipo Alex alipompiga risasi kwa hasira.

Kamanda wa Polisi Kinondoni Ramadhani Kingai amesema bastola aliyokua nayo Alex alikua akiimiliki kihalali lakini akawataka Watu kutokwenda na silaha Bar kunywa pombe hata kama wanazimiliki kihalali kwani wakilewa zinaweza kusababisha madhara kwao au kwa wengine.

.............

MAGARI YAFURIKA MAZISHI YA GIFT ALIYEUAWA KWA KUPIGWA RISASI