Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 19Article 552379

Soccer News of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kikosi cha Taifa Stars hadharani

Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kuingia kambini 24 Agosti Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kuingia kambini 24 Agosti

Shirikisho la Mpira wa Miguu tanzania (TFF), Leo Agosti 19, Limetangaza kikosi cha wachezaji 28 wa Kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Agosti 24, 2021 kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo na Madagascar.

Katika kikosi hicho kimetawaliwa na nyota wengi kutoka timu za Simba (8),Yanga(5) na Azam FC(8),lakini golikipa metacha Mnata pia amejumuishwa licha kuwa hana timu.

Nyota wanaocheza nje wapo wanne ambao ni Mbwana Samatta, Simon Msuva, Nickson Kibabage, na Novatus Dismas.

Coast Union wamemtoa mchezaji mmoja hali kadhalika Gwambina FC pia imetoa mchezaji mmoja.