Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 04Article 541006

Habari za michezo of Friday, 4 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Kikwete azindua uwanja wa kikapu, atema cheche

Kikwete azindua uwanja wa kikapu, atema cheche Kikwete azindua uwanja wa kikapu, atema cheche

Mradi huo unajengwa kwa msaada wa Taasisi ya GOA (Giant of Africa), ambayo inaongozwa na Rais wa klabu ya Toronto Raptors inayoshiriki Ligi ya NBA ya Marekani, Masai Ujiri.

Kikwete alisema mpira wa kikapu hapa nchini utapiga hatua kama kutakua na miundo mbinu mizuri pamoja na walimu wa kufundisha vijana kuufahamu vyema mchezo huo.

"Niwaombe Wana-Kisarawe kukitunze kiwanja hiki pindi kitakapomalizika, kwa sabau uwepo wa kiwanja hiki ni hatua moja zaidi katika kuleta maendeleo ya mchezo huu ambao mimi mwenyewe nimeucheza miaka ya nyuma," alisema Kikwete.

Alisema Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amefanya kazi kubwa kuwashawishi GOA na TBF kuleta mradi huo wa uwanja wilayani huko ili kuchangia kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana.

"Viwanja hivi nimeambiwa vinajengwa na sehemu nyingi Afrika, lakini katika hivyo kimoja kinajengwa Tanzania na ndio hiki pekee, hii ni kazi kubwa imefanywa na Mkuu wa Wilaya (Jokate), ni jukumu letu kukitunza ili kisaidie kuinua mchezo huu," Kikwete alisema.

Pia ameitaka TBF kuandaa mapema timu za vijana zitakazoshiriki mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika ifikapo Agosti, mwaka huu huko Mali ili ziende kufanya vizuri na kuepuka lawama na kufanya maandalizi ya zimamoto.

"Lakini pia niwaombe wenzetu wa GOA kama ambavyo wametusaidia kwenye kiwanja hiki, watusaidie pia katika kutoa mafunzo ya ufundishaji mchezo huu kwa walimu ambao watawafundisha vijana wetu mashuleni," aliongeza Kikwete.

Naye Mkuu wa Shule ya Minaki, Harold Chungu, alishukuru ujenzi wa uwanja huo kuwepo shuleni kwake.

Kwa upande wake Mkandarasi wa uwanja huo, Josephat Abraham kutoka Kenya alisema kama kutakuwa na hali nzuri ya hewa , ujenzi huo utakamilika baada ya miezi mitatu kuanzia leo ambapo wanatarajia kuanza rasmi ujenzi.

Join our Newsletter