Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 26Article 544378

Habari za michezo of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Simba, Azam wajaza uwanja mapema

Simba, Azam wajaza uwanja mapema Simba, Azam wajaza uwanja mapema

MUDA mchache kabla ya mechi ya nusu fainali ya kombe la Azam (ASFC), kati ya Azam na Simba kuanza kwenye uwanja wa Majimaji, Songea tayari mashabiki wamejaa katika majukwaa yote wakisubiri kuanza kwa mtanange huo.

Mwanaspoti imethibitisha hilo saa 7:40 uwanja huo ulikuwa tayari umefurika mashabiki wa timu hizo mbili huku wale wa Simba wakionekana kuwa wengi kuliko wenyeji Azam.

Dakika sita baadae basi msafara wa Azam ukiongozwa na gari la Askari uliingia uwanjani hapo na kuamsha shangwe kutoka kwa mashabiki.

Mbwembwe ziliendelea uwanjani hapo na mashabiki wengine wakiendelea kuingia huku nje foleni ya mashabiki ikionekana kuendelea kuwa kubwa zaidi.

Mtanange huo unayarajiwa kuanza saa 9:30 jiono na mshindi atatinga fainali kukutana na Yanga iliyofuzu jana baada ya kuichapa Biashara United bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliofanyika mkoani Tabora.