Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 12Article 551179

Soccer News of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Kila anaesajiliwa Yanga amefuzu Vipimo" - Daktari Yanga

Vipimo anavyofanyiwa Mchezaji kabla ya Kusajiliwa Vipimo anavyofanyiwa Mchezaji kabla ya Kusajiliwa

Daktari wa klabu ya Yanga, Shecky Mngazija ameudhihirishia Umma wa Watanzania kuwa, kila mchezaji anayesajiliwa na klabu hiyo amepitia hatua ya vipimo na kuiridhisha klabu ndio maana akasajiliwa.

Kauli hiyo imekuja baada ya wadau mbali mbali wa soka nchini, kuhoji kwa nini hakuna taarifa za vipimo katika sajili za Wachezaji zinazoendelea katika timu za ligi kuu hapa nchini Daktari huyo amesema;

"Mimi sio msemaji wa timu lakini kwa uchache tu nikuhakikishie wachezaji wote wanaosajiliwa Yanga wanapimwa,tena sio tu kupimwa bali wanapimwa vipimo vyote vya kawaida mpaka vipimo vya kibingwa" ameeleza Mngazija

"Ninaposema vipimo vya kawaida namaanisha uzito,urefu,macho,damu na vingine vingi wakati vile vya kibingwa ni pamoja na moyo,mapafu kwa ujumla viungo vyote vya ndani" amesisitiza

Kikosi cha wanajangwani kinatarajiwa kusafiri Agosti 15 mwaka huu kuelekea nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya wa Ligi 2021/2022, na wanatarajia kujifua kwa siku 10 kabla ya kurejea Agosti 25 kujiandaa na wiki ya Mwananchi.