Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 29Article 540466

xxxxxxxxxxx of Saturday, 29 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kim aita silaha 27 Stars

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars Kim Poulsen ameita wachezaji 27 kitakachoingia kambini Juni 5, kujiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Malawi.

Akizungumza Dar es Salaam jana Kim alisema anataka kufanya mazoezi kwa sababu wanataka kushinda ndio maana amewaita wachezaji wenye uzoefu na wengine vijana anaowatengeneza kwa ajili ya timu ya baadaye.

“Wachezaji niliowaita naamini wapo vizuri kimbinu, ufundi na kisaikolojia kucheza na kuleta ushindi kwa taifa,” alisema Kim.

Kim ametangaza kikosi hicho jana huku akimjumuisha mshambuliaji wa Mbeya City Denis Kibu kwa mara ya kwanza na kuwaacha wachezaji kama Jonas Mkude, Farid Mussa na Thomas Ulimwengu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Yanga) na Juma Kaseja (KMC).

Mabeki ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, Erasto Nyoni ( Simba), Israel Mwenda wa KMC, Edward Manyama wa Ruvu Shooting, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job (Yanga).

Viungo ni Nickson Kibabaje (Yousssoufia FC- Morocco), Simon Msuva (Wydad AC- Morrocco) Mudathir Yahya (Azam FC), Muzamir Yassin (Simba), Feisal Salum (Yanga), Salum Abubakar, Idd Seleman Nado na Braison Nkulula (Azam FC).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (Fenerbahçe FC-Uturuki), John Bocco (Simba) Abdul Hamis (Coastal Union), Ayoub Lyanga (Azam FC), Denis Kibu (Mbeya City), Meshack Abraham (Gwambina FC), Novatus Dismas (Maccabi Tel Aviv-Israel) na Yusuf Mhili (Kagera Sugar).

Join our Newsletter