Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 24Article 553399

Soccer News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Kinachotuangusha wazawa ni ufinyu wa nafasi" - Wazir Jr

Aliekuwa Mshambuliaji wa Yanga, Waziri Jr Aliekuwa Mshambuliaji wa Yanga, Waziri Jr

Hivi karibuni Mshambuliaji wa Yanga, Waziri Jr aliamua kuvunja mkataba na klabu ya Yanga kutokana kile alichokieleza ni kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara, hivyo anataka kwenda sehemu ambayo atacheza mara kwa mara ili kulinda kipaji chake.

Waziri Jr, aliesajiliwa na Yanga SC kutoka klabu ya Mbao FC, amesema tatizo kubwa la wachezaji wa ndani kushindwa kuonesha uwezo ndani ya Simba na Yanga ni kwasababu ya kutoaminiwa.

"Ndani ya mechi 9 za kwanza nikiwa Yanga sikucheza, nilikuja kupata bahati kucheza mechi ya 10 ambayo ilikuwa dhidi ya KMC na ndio maana nikamwambia Makapu kuwa naenda kufunga leo na nikaandika ujumbe ule wa ''Mwamba wa CCM Kirumba'' na kweli nikafunga ". amesema Wazir Junior

"Changamoto kubwa ya vilabu vyetu ni kukosa watu wa saikolojia labda mpaka kocha aongee na wewe, Nashukuru kocha Nasreddine Nabi kwenye mechi ya Yanga na Simba SC aliniambia sababu za kutocheza na kesho yake nilikuwa wa kwanza kufika mazoezini". amesema