Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541426

Habari za michezo of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kinda Serengeti Boys mambo yamnyookea

Kinda Serengeti Boys mambo yamnyookea Kinda Serengeti Boys mambo yamnyookea

ALIYEKUWA nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, ‘Serengeti Boys’, Mourice Abraham ametarajiwa kuanza kuitumikia Spartak Subotika inayoshiriki Ligi Kuu nchini Serbia kwa mkataba wa miaka minne.

Kiungo huyo ambaye yupo chini ya usimamizi wa Samaplayer Management yupo nchini Serbia tangu Februari mwaka huu katika timu ya vijana ya timu hiyo.

Kampuni inayomsimamia inaongozwa na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na kupitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha moja ya video za mchezaji huyo akiwa mazoezini na timu hiyo nchini Serbia.

Mourice alianzia kucheza katika timu ya vijana chini ya miaka 19 na Agosti ataanza kutumikia timu ya wakubwa.

Samatta aliandika kwenye ukurasa wake kuwa baada ya kustaafu soka ana ndoto nyingi anataka kuzitimiza lakini hawezi kutaja mojamoja kwa sababu inawezekana akataja hiki halafu kesho akaangukia sehemu nyingine.

“Najua watu wengi wanatamani nisaidie vijana kufika angalau sehemu niliyofika, hiyo ni ndoto yangu kusaidia watoto wa kitanzania wenye vipaji kufikia ndoto zao, hilo nitafanya,” alisema Samatta.

Samatta ambaye anachezea Fenerbahçe, Uturuki yupo nchini baada ya ligi kumalizika na sasa yupo kambini na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.

Join our Newsletter