Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554305

Habari za michezo of Monday, 30 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kipa mpya Yanga awakosha mashabiki

Kipa mpya Yanga awakosha mashabiki Kipa mpya Yanga awakosha mashabiki

Kipa Djigui Diarra ameanza vema kwenye kikosi cha Yanga baada ya mechi yake ya kwanza mashabiki kumkubali na kusema walichokisikia kuhusu kipa huyo wameanza kukishuhudia.

Kipa huyo raia wa Mali amewakosha mashabiki wa Yanga baada ya kuokoa hatari baada ya mchezaji wa Zanaco kuwapiga chenga mabeki watatu wa Yanga na kupiga shuti akiwa na kipa na Diarra kudaka.

Tukio hilo lilishangiliwa na maelfu ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Baadhi ya mashabiki baada ya tukio hilo walianza kunfurahia kipa huyo huku wengine wakitania kwamba ni kweli Diarra ana uwezo wa kudaka hata mbegu za ubuyu na si mpira pekee.

"Huyu kipa Yanga tumelamba dume kwa kiwango chake, hapa hatujapigwa," amesema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Soud Juma.

Shabiki mwingine, Jally John amesema Diarra ni kipa wa kimataifa, ana kiwango bora tofauti na waliowahi kupita Yanga misimu miwili iliyopita.

Hata hivyo kocha wa zamani wa makipa, Juma Pondamali amesema kiwango cha kipa huyo kitapimwa baada ya mechi tatu.

"Kwa CV ni kipa mzuri na ameanza vizuri, ila tumuangalie kwa mechi tatu hivi ndiyo tutajua," amesema.