Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585760

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kisa Kumkosa Chama, Wananchi Kusimamisha Nchi

Kisa Kumkosa Chama, Wananchi Kusimamisha Nchi Kisa Kumkosa Chama, Wananchi Kusimamisha Nchi

IKIWA imebaki siku moja kufungwa kwa dirisha la usajili Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema wanatarajia kushtua Tanzania kwa kufanya usajili.

Yanga hadi sasa wamesajili wachezaji wanne dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufungwa kesho wachezaji walio sajiliwa ni Salum Abubakari, Denis Nkane, Abutwali Mshery na Chrispin Ngushi.

Mbatha alisema bado wananafasi ya kusajili kabla ya dirisha halijafungwa watafanya kitu kikubwa ambacho amethibitisha kuwa kitashtua nchi.

“Ndio tumeshakamilisha sajili za wachezaji wanne haina maana kwamba tumeshakamilisha bado kuna nafasi ya kusajii tutasimamisha nchi kwa muda,” alisema na kuongeza kuwa;

“Anaekuja ni mchezaji wa Yanga sitaki kusema ni mzawa au wa kigeni kikubwa subirini mambo yanakuja mashabiki kuweni na amani tunahitaji ushirikiano wetu hatuwezi kuwaangusha,” alisema.