Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 586006

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kisa kipigo Guardiola azinguana na beki wake

Kisa kipigo Guardiola azinguana na beki wake Kisa kipigo Guardiola azinguana na beki wake

ULISHAWAHI kusikia baadhi ya makocha wakubwa duniani wakizinguana na wachezaji wao huku sababu kubwa ikiwa ni kutofuata maelekezo au kusababisha timu kupoteza mchezo, ishu hii ilitokea Jumapili iliyopita kwenye Dimba la Mwembeyanga ambapo kocha wa timu ya Mpira Kazi Jalilu Mussa ‘Guardiola’ alizinguana na beki wake Ally Ally baada ya kutoa boko lililopelekea wapoteze mchezo.

Mpira Kazi walikubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Don Bosco kwenye mchezo uliopigwa wikiendi iliyopita katika Dimba la Mwembeyanga ambapo dakika ya 67 timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 ndipo beki wa kati wa Mpira Kazi, Imma Thiago alishindwa kuokoa mpira wa krosi uliopigwa kuelekea langoni kwao na kusababisha Don Bosco kufunga bao la pili.

Baada ya mchezo Guardiola alionekana kumgombeza Thiago kutokana na uzembe alioufanya ambao uliwagharimu na kujikuta wanapoteza mchezo huo jambo ambalo liliibua pia hasira kwa beki huyo nusura wazichape kavu kavu na kocha wake kabla ya wachezaji kuwaamulia.