Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 31Article 554653

Soccer News of Tuesday, 31 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kiungo Azam aitwa Harambee Stars

Kenneth Muguna, Kiungo wa Azam Kenneth Muguna, Kiungo wa Azam

Kiungo wa Kimataifa wa Kenya na Klabu ya Azam FC, Kenneth Muguna leo ameondoka kwenye kambi ya Azam FC iliyopo Ndola, Zambia kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya Kenya.

Azam ipo Zambia kwa ajili ya maandalizi ya kabla ya msimu ya takribani wiki moja na nusu, ambapo wakiwa huko wamepanga kucheza michezo minne ya kirafiki kabla ya kurejea Tanzania Septemba 5, mwaka huu.

Watakaporejea Azam watakuwa kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, unaotarajiwa kuchezwa kati ya Septemba 10 hadi 12, mwaka huu.

Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema

“Kikosi chetu kinaendelea vizuri na maandalizi ya kabla ya msimu ‘Preseason’ hapa Ndola Zambia".

Katika mchezo wake wa kwanza Azam ilipokea kipigo cha magoli 4-0, Lakini kadri siku zinavyokwenda wanaonekana kupata muunganiko wa kikosi chao, kitu kinachotoa taswira kwamba huenda wakafanya vizuri zaidi msimu huu.

“Tunatarajia kuwa kiungo wetu wa kimataifa wa Kenya Kenneth Muguna ataondoka kambini kwa ajili ya kujiunga na timu ya taifa ya nchi yao.”

Mchezo wa pili Azam FC ilicheza na Kabwe Warriors ambapo ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Prince Dube.