Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 15Article 585949

Soccer News of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kiungo Yanga: Huyu Sakho ni balaa

Pape Ousmane Sakho Pape Ousmane Sakho

KIUNGO mchezeshaji wa zamani wa Yanga, Amri Kiemba, amefurahishwa na kiwango na aina ya uchezaji wa kiungo Msenegali wa Simba, Pape Ousmane Sakho huku akimtabiria makubwa nyota huyo.

Msenegali huyo ameonyesha kiwango bora huku akifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi katika michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo inaendelea huko Unguja, Zanzibar.

Staa huyo hivi sasa ni gumzo kwa mashabiki wa Simba kutokana na kiwango alichokionyesha katika mchezo dhidi Mlandege FC na dhidi ya Namungo FC ambao alitwaa uchezaji bora wa mechi.

Kwa mujibu wa Kiemba ambaye pia amewahi kuichezea Simba kwa mafanikio makubwa, hivi sasa hauwezi kuwataja wacheza muhimu na tegemeo katika kikosi cha Simba bila ya kumtaja Sakho mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao.

Kiemba alisema kuwa kiwango ambacho hivi sasa anakionyesha Sakho, wengi hawakutarajia na kama akiendelea kwa kasi hiyo, basi atafanikisha malengo yake.

Aliongeza kuwa kiungo huyo anatakiwa kuendelea na kasi hiyo mara baada ya kurejea katika Kombe la Shirikisho Afrika, Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

“Kikosi cha Simba kadiri siku zinavyokwenda kinakuwa imara na bora zaidi, mfano mzuri ni huyu Sakho ambaye ameonekana kubadilika na kuonyesha kiwango kikubwa.

“Katika michuano hii ya Kombe la Mapinduzi, Sakho ameonyesha ubora wake, ameonekana mchezaji tegemeo wa kuipa matokeo mazuri timu yake ya Simba.

“Sakho ni mchezaji ambaye wengi hawaku

tarajia kama anaweza kuibeba timu kwenye mabega yake na kuwa mtu muhimu, kutokana na kiwango bora alichokionyesha anaweza akafanya chochote ndani ya uwanja,” alisema Kiemba.