Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573511

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Klopp atoa sababu kulumbana na Arteta

Arteta akizozana na Klopp Arteta akizozana na Klopp

Kocha wa Majogoo wa Jiji, Jurgen Klopp ameelezea kwa kina sababu zilizomfanya kugombana na Mikel Arteta.

Klopp amesema hatua hiyo imekuja kwa sababu raia huyo wa Hispania pamoja na benchi lake la ufundi walitaka Sadio Mane atolewe nje kwa kadi nyekundu, huku Liverpool ikishinda 4-0 dhidi ya Arsenal, Jumamosi.

Mane, ambaye amefunga mabao mengi ya Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace (13) huku Arsenal akiwafunga mara nane, alifunga la ufunguzi kipindi cha kwanza pale kwenye dimba la Anfield, kabla ya Diogo Jota, Mohamed Salah na Takumi Minamino kila mmoja kufunga moja na kujivuta hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi.

Mshambuliaji huyo wa Senegal alifunga bao kwa kichwa muda mchache baada ya makocha hao wawili kutupiana maneno, kwa sababu Mane alionekana kumfanyia faulo, Takehiro Tomiyasu.

Arteta na wasaidizi wake walighadhabika na walipaza sauti kwa mwamuzi kwamba, Mane alimpiga kiwiko mlinzi huyo wa Arsenal.

Klopp naye akajibu mashambulizi kabla ya mwamuzi, Michael Oliver kuingilia kati na kuwaonyesha kadi ya njano makocha wote wawili.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo baada ya mchezo huo, Klopp aliiambia Sky Sports: "Ilikuwa ni tukio ambapo Sadio hakufanya faulo, lakini benchi la Arsenal liliamka na kutaka itolewe kadi nyekundu. Niliwauliza wanataka nini kwenye tukio lile.

"Tulilazimika kumtoa Sadio nje kwenye mchezo dhidi ya Atletico (Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya) kwa sababu nao walitaka apewe kadi ya njano.

"Kwa hakika mwamuzi alifanya vizuri kwenye hali ile, ilistahili kadi ya njano.”