Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 19Article 572863

Soccer News of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Klopp awatetemesha Arsenal kuelekea mechi yao Jumamosi

Liverpool wataikaribisha Arsenal wikiendi hii Liverpool wataikaribisha Arsenal wikiendi hii

Wakali wa soka wanakwambia “mind games” ni mbinu ya mchezo. Jurgen Klopp, Solskjaer, Guardiola na Tuchel ni miongoni mwa makocha wanaotumia mbinu hiyo.

Liverpool watakua uwanjani Jumamosi hii kuwaalika Arsenal. Huu ni mchezo ambao, kwa miaka mingi matokeo ya 0-0 sio kitu kirahisi kutokea. Iwe ni Anfield au Emirates, lazima nyavu zote zitikisike.

Mikel Arteta hajapoteza mchezo kati ya mechi 8 walizocheza hivi karibuni. Klopp anaingia kwenye mchezo huu akiwa ametokea kupigwa 3-2 na West Ham United pale London Stadium.

Hakika, ni timu mbili zinazoingia uwanjani zikiwa na hisia mbili tofauti. Hisia za timu gani zitageuka kuwa motisha au makaa ya moto? Arteta anajua kabisa, anaingia kwenye uwanja ambao sio mrahisi. Amekiri hili kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mapema Ijumaa hii.

“Kupata matokea dhidi ya Liverpool wakiwa Anfield, unahitaji kucheza katika kiwango chako cha juu zaidi”

Kauli ya Arteta inaongezewa nguvu na kama kumbusho kwao kutoka kwa Jurgen Klopp.

Kocha huyu wa Kijerumani amekiri kuwa, Liverpool bado haijapata matokeo mazuri ambayo pengine wanaridhika nayo sana lakini, pamoja na yote – Jurgen amesema,

“Arsenal ni timu nzuri ya soka lakini tupo [Liverpool] Anfield na tunatakiwa kuonesha hilo”.