Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 560017

Habari za michezo of Monday, 27 September 2021

Chanzo: eatv.tv

Kocha Taifa Stars alia na vilabu vya Simba, Yanga

Kocha Taifa Stars alia na vilabu vya Simba, Yanga Kocha Taifa Stars alia na vilabu vya Simba, Yanga

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amevitupia lawama vilabu vinavyowasajili wachezaji mara tu anapowaita kwenye kikosi chake

Kocha huyo raia wa Denmark ameyasema hayo leo wakati akiweka hadharani majina ya wachezaji 25 ambao wataingia kambini Oktoba 3,2021 kujiwinda na michezo miwili dhidi ya Benin ambayo ni ya kuwania kufuzu Fainali za kombe la Dunia huko nchini Qatar,2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Poulsen amesemema hafurahishwi na kitendo cha baadhi ya vilabu vya Ligi Kuu Tanzania bara kuwasajili wachezaji pindi tu wanapoitwa kwenye timu ya Taifa kwakuwa hawapewi nafasi ya kucheza katika vilabu vyao kiasi cha kumpa wakati mgumu katika uteuzi wake kwa awamu nyingine huku akitolea mfano wachezaji Yusuph Mhilu na Israel Mwenda waliojiunga na Simba.

Katika kikosi chake , Poulsen amemrejesha kikosini kiungo mwandamizi, Jonas Mkude ambaye kwa muda mrefu alikuwa nje ya timu ya Taifa huku ikiaminika ni kutokana na sababu za utovu wa nidhamu katika klabu yake.

Taifa Stars yenye alama 4 katika kundi J baada ya michezo miwili, itakabiliana na Benin Oktoba 7 na 10 katika michezo ambazo zitatoa taswira ya Tanzania kufuzu kwenye Fainali za kombe la Dunia.