Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 21Article 573208

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kocha Uruguay atimuliwa

Oscar Tabarez Oscar Tabarez

Timu ya taifa ya Uruguay imemfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wao Oscar Tabarez baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka 15.

Kocha huyo wa miaka 74 alirejea Uruguay kwa mara ya pili mwaka 2006 baada ya kuwahi kufanya kazi na timu hiyo mwaka 1988-90 baada ya kushindwa kufuzu kombe la Dunia mwaka huo.

Katika michuano ya kombe la Dunia la mwaka 2010 ilimaliza katika nafasi ya 4 na kupata Copa America mwaka 2011 lakini licha ya kupata mafanikio kama hayo ameshindwa kufuzu moja kwa moja kombe la Dunia 2022 baada ya kukubali kichapo cha 3-0 kutoka kwa Bolivia siku ya Jumanne.

Tabarez amefungishwa vilago na AUF baada ya kushinda michezo minne kutoa sare nne na kufungwa mara sita katika mechi 14 wakikaa katika nafasi ya saba.

Taarifa ya shirikisho la soka la nchini Uruguay AUF ilisema: “Haya ni maamuzi magumu kutokana na kinachoendelea kwaajili ya malengo tuliyonayo hapo baadaye.

“Tuna elezea heshima zetu kwa Tabarez Taaluma na kujitolea kwa kipindi kirefu.