Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 02 21Article 525709

Soccer News of Sunday, 21 February 2021

Chanzo: habarileo.co.tz

 Kumbe Kaze aliwasoma Mtibwa mapema 

 Kumbe Kaze aliwasoma Mtibwa mapema   Kumbe Kaze aliwasoma Mtibwa mapema 

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema ushindi wa bao 1-0 walioupata jana dhidi ya Mtibwa Sugar umetokana na kuwasoma wapinzani hao kwa muda mrefu ndani na nje ya uwanja.

Kaze amebainisha hayoalipohojiwa na chombo kimoja cha habari jijini Dar es salaam.

"Niliwapa maelekezo wachezaji wangu kupambana na kutumia akili katika kusaka ushindi kwakuwa Mtibwa ni timu yenye uzoefu katika kusaka ushindi ndani na nje ya uwanja” amesema Kaze.

Katika mchezo huo Yanga ilipata bao dakika ya 73 lililofungwa na Carlos Carlinhos aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ditram Nchimbi.

Baada ya ushindi huo, Yanga imeendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 49 baada ya kucheza mechi 21.

Join our Newsletter