Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 11Article 584866

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kumbe tumepigwa kwa Phiri, Zanaco yatoa tamko

Phiri anahusishwa na vilabu vya Simba na Yanga Phiri anahusishwa na vilabu vya Simba na Yanga

Simba na Yanga zimekuwa zikipigana vikumbo kuwania saini ya Phiri, huku taarifa nyingine zikisema tayari ameshamalizana na Vijana wa Jangwani ili atue mwishoni mwa msimu huu na nyingine zikisisitiza kuwa jamaa atavaa uzi wa mitaa ya Msimbazi.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Zanaco, Roy Mutombo akizungumza kwa njia ya simu jana asubuhi alikiri klabu yao imepokea ofa mbili za kutoka Simba na Yanga.

Mutombo alisema, Yanga ndio iliyokuwa ya kwanza kumtaka Phiri tangu mapema mwaka jana, lakini baadaye kasi yao ikapungua ndipo wakaibuka Simba baadaye.

“Ukweli ni kwamba tumepokea ofa mbili za kuhitajika kwa Phiri kimaandishi kutoka kwa klabu zote mbili za hapo kwenu Tanzania, yaani Simba na Yanga,” alisema Mutombo

Mkurugenzi huyo akaongeza kwa kusema lakini ghafla hivi karibuni mabosi wa Yanga walirudi tena kwa nguvu katika kufufua dili hilo na bado wanaendelea kuongea nao kwa kuwa Phiri bado yuko katika mkataba.