Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 06 07Article 541429

Habari za michezo of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kumekucha uchaguzi TFF

Kumekucha uchaguzi TFF Kumekucha uchaguzi TFF

FOMU za kuwania urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) zitaanza kutolewa kesho kwa Sh 500,000 huku wajumbe wa kamati ya utendaji wakichukua kwa Sh 200,000.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Kiomoni Kibamba utoaji fomu mwaka huu utafanyika kwa siku nne kuanzia Juni 8- 12 katika Ofisi za Shirikisho zilizopo Karume, Ilala lakini pia unaweza kupata kupitia tovuti ya TFF.

‘Kila mtu ambaye anaamini ana sifa za kugombea nafasi zilizoainishwa anakaribishwa kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania kuchaguliwa, fomu kwa urais ni Sh 500,000 na mjumbe wa kamati ya utendaji Sh 200, 000,” alisema Wakili Kiomoni.

Wakili Kiomoni alisema fedha za kuchukulia fomu zinatakiwa kulipwa benki ya CRDB tawi la Holland House, namba 01j1019956600, jina la akaunti Tanzania Football Federation na baada ya kufanya malipo muhusika anapaswa kuambatanisha risiti yake kwenye fomu.

Uchaguzi Mkuu wa TFF, unatarajiwa kufanyika Agosti 7, jijini Tanga ambapo viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa miaka minne.

Mara ya mwisho Uchaguzi Mkuu kufanyika ulifanyika Agosti 12, 2017 Dodoma, ambapo Wallace Karia alifanikiwa kupata kura 95 kati ya kura 127, akifuatiwa na Ally Mayay aliyepata kura tisa sawa Shija Richard.

Join our Newsletter