Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 27Article 559987

Soccer News of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kumuona Messi akichezea PSG sio kitu cha Kawaida- Guardiola

Nyota mpya wa PSG, Lionel Messi anatarajiwa kuwepo dimbani kesho Nyota mpya wa PSG, Lionel Messi anatarajiwa kuwepo dimbani kesho

"Ilikuwa mshangao kwa kila mtu (kwamba Lionel Messi aliondoka Barcelona) lakini ndivyo ilivyotokea" amesema Pep

Messi anatarajiwa kurejea kutoka katika majeraha na kushiriki mchezo wa Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne dhidi ya Manchester City kwenye Uwanja wa Parc des Princes.

Pep Guardiola , akiwa na Messi ameshawahi kuiongoza Barcelona kushinda ubingwa wa Ulaya mara mbili.

Hivyo atapambana na mchezaji wake nyota wa zamani ambae kwa sasa anakipiga PSG pindi timu hizo zitakapokutana siku ya Jumanne katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa.

"Ni muda mrefu umepita, hakuna aliedhani lakini imetokea nina imani ana furaha ndani ya kikosi cha PSG".

"Kipaji chake ni cha kipekee, tunatumai kesho atacheza kwa faida ya klabu yake" amesema Pep

Messi amekosa mechi mbili za mwisho za PSG kutokana na maumivu, lakini amefanya mazoezi kuelekea mchezo wa Man City.