Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573361

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kuondoka kwa Ole, manufaa kwao

Jesse Lingard Jesse Lingard

Kuondoka kwa Kocha Ole Gunnar Solskjaer ndani ya kikosi cha Manchester United ni wazi kunatoa nafasi kwa baadhi ya wachezaji sasa kuwa na imani kuwa wanaweza kuamka na kufanya kweli huku wengine wakiwa na uwezekano wa kuwa na maisha magumu.

Wachezaji wanaoweza kuwa na matumaini mapya kwa maamuzi ya kufukuzwa kwa Ole ni hawa hapa:

Donny van de Beek Ameshindwa kuwa na uhakika wa namba, ujio wa kocha mpya utamuamsha kupambana zaidi.

Edinson Cavani Mkongwe huyu amekuwa na msaada mkubwa lakini hakuwa anapata namba ya uhakika.

Jadon Sancho Alisajiliwa kwa mbwembwe nyingi na dau kubwa lakini ameshindwa kuwa na maisha mazuri kwa kukosa namba ya uhakika.

Nemanja Matic Ni mkongwe, anapopangwa amekuwa akionyesha ubora wa juu, lakini hakuwa na namba ya uhakika kikosini.

Eric Bailly Ni beki mzuri, mpambanaji lakini Ole hakupendelea kumtumia mara kwa mara.

Jesse Lingard Alitolewa kwa mkopo msimu uliopita, akawasha moto hasa, aliporejeshwa United, Ole hakutaka kumuuza, akambakisha kikosini lakini hakumpa uhakika wa namba.