Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 23Article 553168

Soccer News of Monday, 23 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kutokana na ufinyu wa ratiba hakuna "Azam Festival"

Afisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria (zaka zakazi) Afisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria (zaka zakazi)

Baada ya kujifua vya kutosha jijini Dar es Salaam, kikosi cha Azam FC kimepaa leo kwenda Ndola, Zambia kuweka kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa, huku ikipiga chini tamasha lao lililoasisiwa mwaka jana, ambalo awali lilipangwa lifanyike Septemba 5.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, timu hiyo itaweka kambi ya wiki moja na itacheza mechi za kirafiki za kujipima nguvu zisizopungua nne na timu za huko.

Zakazi alisema mchezo wao wa kwanza utakuwa dhidi ya Red Arrows na itapigwa keshokutwa, kisha Agosti 29 itavaana na Zanaco, kabla ya Septemba 2 kuwavaa Forest Rangers na siku inayofuata watamalizana na Zesco United.

Baada ya mechi hizo, Azam itarejea nchini kuwahi pambano lao la mkondo wa kwanza la Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed SC ya Somalia litakalochezwa kati Septemba 10- 12.