Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 07 12Article 546583

Soccer News of Monday, 12 July 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kwa Kaseja msasubiri sana

Kwa Kaseja msasubiri sana Kwa Kaseja msasubiri sana

LICHA ya kusakamwa, lakini ubora wa kipa Juma Kaseja akiwa langoni umemfanya kuendelea kuwakimbiza wenzake, akitajwa kuwa ndiye kipa bora mpaka sasa hapa nchini.

Aishi Manula ndiye anayetajwa kuwa ‘Tanzania One’, lakini nyota wa zamani wa kimataifa aliyewahi kukipiga Simba na Yanga, Akida Makunda amemtaja Kaseja kuwa ndiye anayestahili kwa ubora alionao licha ya umri kumtupa mkono.

Makunda aliliambia Mwanaspoti jana kuwa, mpaka sasa Kaseja ndiye namba moja halafu wengine wanafuata licha ya kuwa ni wazuri.

“Kaseja kwangu atabaki na ataendelea kuwa namba moja kwa makipa, japo wengine ni wazuri pia ila namuelewa zaidi huyo jamaa,” alisema Makunda.

Makunda alisema kila mtu ana mtazamo wake, ila yeye anaona kitu kikubwa kwa kipa huyo aliyeichezea Simba na Yanga ambaye amezichezea timu hizo kwa mafanikio makubwa.