Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 20Article 552682

Soccer News of Friday, 20 August 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

"Kwa usajili huu, mtusamehe tu yaani" - Mwamnyeto

Beki wa Yanga na Nahodha msaidizi, Bakari Mwamnyeto Beki wa Yanga na Nahodha msaidizi, Bakari Mwamnyeto

Nahodha msaidizi wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ameiambia Mwanaspoti kwamba kama kuna wakati Yanga imesajili timu bora basi ni sasa.

Mwamnyeto ambaye sio mtu wa kuongea sana amesema karibu idara zote zimesajiliwa vyema wakiongezwa watu hasa waliostahili kuingia wakiwa na ubora mkubwa.

“Huu usajili uliofanyika safari hii ni kama funga kazi, hakuna tena timu ya kutufanya tukose mataji, huu ndio wakati ambao viongozi wamesajili watu wa kweli hasa,” amesema Mwamnyeto ambaye ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union.

“Ukiangalia kila eneo kumeletwa watu hasa, washambuliaji waliokuja ni wazuri sana, viungo wa pembeni nao ni wakali ukiongeza na wale wa kati, haya huku kwenye ulinzi nako kuna watu wa maana,” amesema.

Ameongeza, hata kama kuna timu zitakuwa zimejiandaa vyema lakini msimu ujao kwa timu waliyonayo hakuna sababu ya wao kukosa mataji na kwamba kwasasa wanajipanga vyema ili wawe tayari kwa ushindani.

“Najua kila timu inajipanga sawa, lakini huku kwetu tuko sawasawa kuhakikisha mataji tunayachukua msimu ujao.”