Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 30Article 554272

Soccer News of Monday, 30 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Kweli Yanga wana Watu

Umati wa Mashabiki wa Yanga waliofurika katika Uwanja wa Mkapa Umati wa Mashabiki wa Yanga waliofurika katika Uwanja wa Mkapa

Kweli Yanga wana watu, ndiyo kauli unayoweza kusema kwa sasa baada ya umati mkubwa kufurika kuja kushuhudia kilele cha "Wiki ya Mwananchi".

Mpaka kufikia sasa Uwanja umetapika huku zile "Sapraizi za kidunia" zilizoahidiwa na Msemaji wa Yanga, Haji Manara ikiwa bado haijaoneshwa je patatosha leo?

Wakati ndani kukiwa hivi bado nje katika milango ya kuingilia watu wamefurika wakitaka kuingia ndani kwa maana hiyo unaweza kuona ni kiasi gani Yanga wana mtaji mkubwa wa Mashabiki.

Kwa taarifa yako tu mpaka wakati huu lile zoezi kubwa linalogusa mioyo ya watu la utambulisho wa kikosi cha msimu mpya cha Yanga bado na Kile kipute cha Yanga dhidi ya Zanaco pia bado.