Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 22Article 573463

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Lakers Wapindua Meza Kwa Piston

LA Lakers vs Detroit katika purukushani uwanjani LA Lakers vs Detroit katika purukushani uwanjani

Ligi ya NBA imeendelea leo alfajiri. Timu kadhaa zilikua uwanjani kutafuta pointi muhimu kwenye vilabu vyao. LA Lakers wamefanya yao dhidi ya Detroit Pistons.

Licha ya kuzidiwa kwa pointi 17, Lakers walirejea uwanjani na kupindua meza ya matokeo kwa ushindi wa pointi 121-116. Antony Davis akipachika jumla ya pointi 30 akishirikiana vyema na Russell Westbrook aliyepachika pointi 26.

Kwa mara ya pili kwenye historia yake ndani ya NBA, LeBron James alitolewa uwanjani baada ya kucheza madhambi dhidi ya Isiah Stewart ambaye pia alitolewa nje baada ya kutaka kulipa kisasi.

Katika michezo mingine iliyochezwa usiku wa kuamkia leo, Clippers wameshinda kwa pointi 97-91 dhid ya Mavericks, Suns wamewafunga Nuggets kwa pointi 126-97, Bulls wameshinda kwa pointi 109-103 dhidi ya Knicks na Warriors wamewafunga Raptors kwa vikapu 119-104.