Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 11 18Article 572503

Mpira wa Kikapu of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: eatv.tv

Lebron James kurejea hivi Karibuni NBA?

Lebron James kurejea hivi Karibuni NBA? Lebron James kurejea hivi Karibuni NBA?

Nyota wa Los Angeles Lakers, Lebron James anatazamiwa kurejea tena kwenye court alfajiri ya kuamkia Ijumaa ya kesho Novemba 19, 2021 wakati timu yake itakapocheza dhidi ya Bolton Celtics kwenye NBA baada ya kukosekana tokea Novemba 2, 2021.

Lebron ambaye alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya misulii na ugonjwa wa tumbo amekosekana katika michezo 10 ambayo Lakers wamecheza wakishinda michezo 4 na kufungwa 6 huku Lebron akikosa michezo 8 mfululizo.

Licha ya kufanya mazoezi ya pekeeake akisimamiwa na kocha wake msimamizi, Phil Handy, lakini Lebron alishindwa kuwa sehemu ya mchezo ambao alfajiri ya leo Lakers imefungwa kwa alama 109-102 dhidi ya Mabingwa watetezi Milwaukee Bucks.

Kipigo hiko ni cha 8 kwa Lakers ambao wameshinda  michezo 8 katika michezo 16 ya NBA msimu huu na kushika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa upande wa Western Conference na wapinzani wake Golden State Warriors wakiwa vinara.