Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 21Article 558802

Soccer News of Tuesday, 21 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Lengo letu ni kuhakikisha tunabeba ubingwa" Ruvu Shooting

Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire

Klabu ya Soka ya Ruvu Shooting yenye makazi yake Mlandizi mkoani Pwani, imesema wamejipanga kuhakikisha msimu unaoanza wa ligi wanakwenda kuwa Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara 2021/2022.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Afisa habari wa klabu hiyo Masau Bwire amesema anafahamu wengi hawawezi kuamini hili lakini watakwenda kujionea wenyewe upinzani utakaotolewa na Ruvu Shooting katika Ligi.

"Tanzania imezoeleka mnapoingia katika kucheza mpira kugombania ubingwa, anakuwa ashajulikana kama sio Simba ni Yanga, sasa sisi tunakuja na dhana tofauti kabisa na mitazamo hiyo" amesema masau

"Tutawasumbua sana hao mnaodhani ndio wenye mamlaka ya Ubingwa wa nchi hii, tunataka tuanze na wengine wafuate nyuma yetu wanaodhani ni wachanga au wadogo, sisi kama Ruvu Shooting tunasema udogo huo hatuna" amesisitiza masau

"Katika upande wa huduma tunawashukuru sana Uongozi wetu kwa kuwa ndio wanaotupa kiburi cha kuhakikisha tunakua na malengo makubwa kama haya"

Aidha masau amesema analishukuru jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia makampuni yake tanzu kwa kutoa udhamini mnono kwa Ruvu Shooting.

Masau pia ametambulisha Tamasha la Ruvu Shooting, ambalo litafanyika tarehe 25 mwezi huu na linafahamika kama "Usiku wa Ruvu Shooting"

Kabla ya siku husika watafanya shughuli mbali mbali za kijamii na pia katika maandalizi ya Siku hiyo watakua na mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandizi Kombaini.