Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 17Article 558121

Soccer News of Friday, 17 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Ligi Kuu Zanzibar kuanza Octoba 25

Mjumbe Bodi ya Ligi Mohammed Masoud (Kushoto), M/kiti wa Kamati ya Mashindano, Ali Bakari (kati) Mjumbe Bodi ya Ligi Mohammed Masoud (Kushoto), M/kiti wa Kamati ya Mashindano, Ali Bakari (kati)

Msimu mpya wa Soka la Zanzibar kwa Mwaka 2021-2022 unatarajiwa kuanza Oktoba 25, 2021 kwa kuchezwa Ligi mbali mbali ikiwemo Ligi Kuu Soka ya Zanzibar (ZPL) na Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwa niaba ya Bodi ya Ligi kuu ya Zanzibar kwa kushirikiana na Kamati ya Mashindano, Mjumbe wa Bodi ya Ligi, Mohammed Masoud amesema Msimu mpya utaanza Oktoba 25, 2021 ambapo Dirisha la Usajili linafunguliwa kuanzia Septemba 20, 2021 na litafugwa Oktoba 11, 2021 na Usajili utafanywa kwa njia ya Kimtandao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Ali Bakari "Cheupe" amesema Msimu huu Ligi Kuu Soka ya Zanzibar utajumuisha jumla ya timu 16 zikiwemo 12 kutokea Kisiwani Unguja na timu 4 kutokea Kisiwani Pemba.

Timu 16 zitakazocheza Ligi Kuu Soka ya Zanzibar (ZPL) Msimu mpya wa mwaka 2021-2022 ni Mabingwa Watetezi KMKM, Zimamoto, KVZ, Mafunzo, JKU, Kipanga, Malindi, Mlandege, Polisi, Black Sailors, Uhamiaji, Taifa ya Jang'ombe, Kisiwani Fc, Yosso Boys, Selem View na Machomane.