Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 05 26Article 539980

Boxing News of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Live: Kiduku, Dullah Mbabe Wakisaini Mkatataba Wa Kugombea Toyota Crown

Live: Kiduku, Dullah Mbabe Wakisaini Mkatataba Wa Kugombea Toyota Crown Live: Kiduku, Dullah Mbabe Wakisaini Mkatataba Wa Kugombea Toyota Crown

Live: Kiduku, Dullah Mbabe Wakisaini Mkatataba Wa Kugombea Toyota Crown May 26, 2021 by Global Publishers

MABONDIA Twaha Kiduku na Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, wanatarajia kutambulishwa na kusaini mikataba leo Jumatano katika Uwanja wa Las Vegas, Mabibo jijini Dar.

Kiduku na Dullah Mbabe wanatarajia kusaini mikataba hiyo na kutambulishwa kwa pambano la Usiku wa Deni kupitia Kampuni ya Peak Time Sports Agency chini ya udhamini wa +255 Global Radio, Gazeti la Spoti Xtra, Maziwa ya Asas, Maji ya Afya, Premier Bet, Kebbys Hotel, Creative Bees, Smart Gin na Azam Tv, Good Hope Laboratory na Jembe Energy Drink.

Akizungumza na Championi Jumatano,Mkurugenzi wa Peak Time Sports Agency, Kepteni Seleman Semunyu alisema kuwa, wamebadilisha kutoka jana hadi leo kutokana na kuingiliana kwa matukio na baadhi ya wadhamini wa pambano hilo.

“Ni kweli tulipanga siku ya jana kutambulisha na kutangaza pambano la ‘Pay Back’ Usiku wa Deni pale katika Uwanja wa Las Vegas ikiwa ni kutambulisha mabondia lakini kwa sasa tutafanya tukio hilo siku ya Jumatano (leo) kutokana na kuingiliana kwa matukio ya baadhi ya wadhamini wetu.

“Lakini nje ya hapo ratiba yetu kwa siku ya Jumatano ipo sawa na tunarajia tukio la kesho (leo) litakuwa kubwa kutokana na maandalizi yalivyofanyika kwa kuwa Twaha Kiduku na Dullah Mbabe watakuwepo kwa ajili ya jambo hilo,” alisema Kepteni Semunyu.