Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 09 29Article 560266

Soccer News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Liverpool, Atletico mambo safi UEFA

Pilika pilika za Michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Pilika pilika za Michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Majogoo wa Jiji kutoka Merseyside, Klabu ya Liverpool wanaendelea kuonesha ukongwe wao katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya usiku wa Jana kuibuka na ushindi mnono ugenini.

Liverpool walisafiri mpaka nchini Ureno kupambana na FC Porto katika mchezo wa kundi B, na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 5-1.

Magoli ya Liverpool katika mchezo huo yamefungwa na Sadio mane 45', Mohamed Salah aliefunga magoli mawili 18' na 60' na Kiungo mshambuliaji wa Brazil Firmino ambae alianzia benchi, nae akifunga magoli mawili 77' na 81'.

Ushindi huo unawaweka Liverpool kileleni mwa Kundi B, wakiwa na pointi 6 baada ya kucheza michezo miwili na kushinda michezo yote.

Katika mchezo mwingine wa Kundi B, AC Milan walipoteza mechi ya pili mbele ya Atletico Madrid kwa magoli 2-1.