Uko hapa: NyumbaniMichezo2021 08 15Article 551590

Soccer News of Sunday, 15 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Liverpool, Chelsea zang'ara EPL

Winga wa Liverpool, Mohamed Salah akifunga bbao la tatu dhidi ya Norwich Winga wa Liverpool, Mohamed Salah akifunga bbao la tatu dhidi ya Norwich

Liverpool na Chelsea zimetakata katika mechi zao za ufunguzi wa ligi kuu england baada ya wote kuibuka na ushindi mnono.

Katika mechi ya jioni Chelsea iliwakaribisha timu ya Crystal Palace katika dimba la Stamford Bridge na kuibuka na Ushindi wa mabao 3-0.

katika ushindi huo magoli ya Chelsea yamefungwa na M.Alonso,Pulisic na kinda gumzo kwa sasa Trevoh Chalobah.

Katika mechi ya mwisho kwa siku ya jumamosi imepigwa majira ya saa 1:30 imwwakutanisha majogoo wa Jiji Liverpool waliokuwa ugenini kumenyana na Norwich City katika dimba la Carrow Road na mpaka refarii anapuliza kipenga cha mwisho liverpool wameibukia na Ushindi wa mabao 3-0 magoli yaliyofubgwa na Diogo Jota,Firmino na Mohamed Salah.

Ligi hiyo itandelea kesho ambapo kutakua na mechi kubwa kati ya Totenham Hotspurs watakaowakaribisha vijana wa Kocha Pep Guardiola.