Uko hapa: NyumbaniMichezo2022 01 14Article 585907

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Liverpool: Tunaweza Bila Salah na Mane?

Liverpool inawakosa nyota watatu ambao ni Salah, Mane na Keita Liverpool inawakosa nyota watatu ambao ni Salah, Mane na Keita

Wakati soka barani Ulaya likiendelea, AFCON nayo inaendelea mwezi huu. Liverpool wanaanza kuipata ladha halisi bila ya Mo Salah na Sadio Mane.

Salah, Mane na Keita ni wachezaji watatu wanaokosekana kwenye kikosi cha Liverpool kutokana na ushiriki wao kwenye mashindano ya AFCON mwezi huu.

Ni dhahiri, kukosekana kwa wachezaji hawa, kumepunguza makali ya The Reds ambao mchezo dhidi ya Arsenal ulionesha kile kinachokosekana kwenye timu hiyo.

Licha ya kutawala mchezo kwa 80%, wakiwa Anfield, The Reds walifanikiwa kupiga mkwaju mmoja tu uliolenga goli. Pamoja na Arsenal kupata kadi nyekundu na kucheza muda mrefu wakiwa pungufu, vijana wa Klopp hawakuwa na makali yeyote mbele ya ukuta wa Mikel Arteta.